Nguvu ya Mkristo kufanya lo lote afanyalo hutoka kwa Bwana. Hii nguvu ni Roho wa Mungu ambayo pia hujulikana kama Mkono wa Bwana au Roho Mtakatifu na katika Biblia huwakilishwa kwa picha ya mafuta, yaani upako. Hivyo Kumbukumbu la Torati 8:18 inavyosema "Bali utamkumbuka Bwana, Mungu wako, maana ndiye akupaye nguvu za kupata utajiri; ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama hivi leo" inamaanisha Mungu anawapa upako wa kupata utajiri. Upako huu ni kwa ajili ya Wakristo pia, watu wa Agano Jipya, lakini wengi hawajui kuhusu upako huu achilia mbali namna ya kuutumia. Kitabu hiki kinafafanua fundisho hili na kuonyesha ni wapi ambapo Wakristo wanashindwa kutumia upako wa kupata utajiri kubadilisha maisha yao kiuchumi.